Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Jeshi
la Polisi Mkoani Mbeya limetoa rai kwa wafuasi wa vyama vishiriki
katika uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu kujiepusha kufika katika kituo
cha kupigia kura wakiwa wamevaa nguo zenye picha za wagombea, maneno au
nembo ama rangi za chama cha siasa.
Aidha wametakiwa , kuepuka
kutumia uvumi, maneno ya uongo, hisia au visingizio vyenye lengo la
kuwazuia wengine kwenda kupiga kura.
Pia amewataka kuepuka
kufanya kampeni katika kituo cha kupigia kura iwe kwa maneno ya
ushawishi au kwa kuonyesha ishara ya chama fulani cha siasa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani humo
Ahmed Msangi amesema nivema kila mwananchi anae stahili kupiga kura
ahakikishe anafuata taratibu hizo ili kujiepusha na vitendo vya uvujifu
wa amani katika siku hiyo muhimu.
Amesema vyema kila mwananchi
kupiga kura kwa kutumia jina na kitambulisho chake na sio cha mtu
mwingine, aliyekufa au mgonjwa, kuepuka kufanya fujo ama vurugu katika
kituo cha kupigia kura.
Aidha amesisitiza kuwa kila mpiga kura
mara baada ya kupiga kura kuondoka kwenye kituo cha kupigia kura na
kuendelea na shughuli nyingine kwani ni kosa kupiga kura na kuendelea
kubaki katika eneo la kituo cha kupigia kura.
Amesema ni wajibu
wa jeshi la polisi kuwalinda maofisa wanaosimamia uchaguzi, kuhakikisha
kwamba zoezi la upigaji kura linaenda sawa, bila vikwazo au bughudha na
kuhakikisha vifaa vya kupigia kura viko salama.
Kwa mkoa wa mbeya
tuna jumla ya majimbo 13 ya uchaguzi, vituo 3,899 vya kupigia kura,
kila kituo kitalindwa na askari ili kuhakikisha suala la ulinzi na
usalama linaimarishwa kwa kipindi chote cha zoezi la kupiga kura,
kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Msangi amesema
Jeshi la polisi mkoa wa mbeya limejipanga kuimarisha ulinzi katika
maeneo yote ikiwa ni pamoja na vituo vya kupigia kura sanjali na kuwepo
kwa na doria za magari, pikipiki, mbwa na askari ambao watakuwa
wakitembea huku na kule kwa lengo la kudhibiti vitendo vyovyote vya
uvunjifu wa amani.JAMIIMOJABLOG
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni