Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Mh. Emmerson Mnangagwa akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa tano
wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo endelevu barani Afrika
unaoendelea muda huu Victoria Falls-Zimbabwe. Ambapo amezitaka nchi za
Afrika kuendelea kushikamana katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi pamoja na ukuaji wa uchumi. (Picha zote na Andrew Chale,
Modewjiblog)
Baadhi
ya washiriki wa mkutano mkubwa wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi na
Maendeleo endelevu barani Afrika unaoendelea muda huu Victoria
Falls-Zimbabwe wakifuatilia mada mbalimbali kwa watoa mada (hawapo
pichani). Mada mbalimbali za kujadili juu ya Afrika hatua ya kuchukua
kuelekea mkutano mkubwa wa Dunia wa COP 21, utakaofanyika nchini Paris,
Ufaransa mwishoni mwa mwaka huu.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[VICTORIA
FALLS-ZIMBABWE] Mkutano mkubwa wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi na
Maendeleo endelevu barani Afrika umeanza rasmi leo katika mji wa Kitalii
wa Victoria Falls, Nchini hapa huku ukishirikisha watu mbalimbali
kutoka nchi za Afrika na nje ya Afrika.
Washiriki
wanaoshiriki mkutano huu unaondelea hapa ni pamoja na wadau wa mambo ya
mazingira, wanaharakati, taasisi binafsi, Serikali, Mashirika ya
kijamii, Wafanyabiashara, wanahabari na viongozi wa Kiserikali na
wanasiasa katika kujadili kwa pamoja.
Mkutano
huo umeanza rasmi leo Oktoba 28-30, wiki hii umeandaliwa kwa
ushirikiano wa mashirika mbalimbali ikiwemo UNECA, Serikali ya Zimbabwe
pamoja na mashirika mengineyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni