MAREHEMU PAUL WALKER AINGIZA FEDHA NYINGI LICHA YA KUTOKUWEPO DUNIANI

Nyota wa filamu ya Fast & Furious marehemu Paul Walker ameingia katika orodha ya jarida la Forbes ya mastaa waliokufa wanaoingiza fedha nyingi.

Walker, aliyekufa kwa ajali ya gari mwaka 2013, ameingiza dola milioni 10.5, katika mwaka uliopita na anashika nafasi ya tisa.

Mfalme wa Pop marehemu Michael Jackson anashika nafasi ya kwanza kwa mwaka watatu mfululizo, akiingiza dola milioni 115, ikiwa ni pungufu na mapato ya mwaka jana milioni 140 mwaka 2014.

Marehemu Elvis Presley anashika nafasi ya tatu kwa mastaa waliokufa lakini bado wanaingiza fedha kwa kupata dola milioni 55.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni