TOTO YAPATA VIONGOZI WAPYA

Klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza leo imefanya uchaguzi wake wa kuchagua viongozi, kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika nafasi ya Mwenyekiti na Wajumbe wawiliwa Kamati ya Utendaji uliomalizika katika hali ya amani na utulivu mkubwa.

Katika uchgauzi huo Godwin Aiko amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu hiyo yenye makao yake makuu mitaa ya kishamapanda, huku Lushinge Lushinge na Timoth Kilumule wakichaguiwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, mwanasheria Aloyce Komba na Domina Madeli.

TFF inawapongezai viongozi wapya waliochaguliwa na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni