WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema hajahama Chama cha Mapinduzi (CCM) kama
ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi watu na mitandao ya kijamii kwamba
amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti jana (Jumamosi,
Oktoba 24, 2015) na wakazi wa majimbo ya Mpanda Mjini na Kavuu kwenye
mikutano minne ya hadhara iliyofanyika katika kata za Kakese, Kibaoni,
Usevya na Majimoto wakati akifunga kampeni za uchaguzi mkoani Katavi.
“Kuna picha zimesambaa mitandaoni zinadai nimehamia CHADEMA. Hivi
kweli, sasa hivi nahamia huko ili iwe nini?” Alihoji na kushangiliwa na
wakazi wa majimbo hayo.
Alisema picha wanazozisambaza ni za mwaka 2012 ambazo zilipigwa wakati
akionyesha kwa wananchi moja ya kadi alizopokea kutoka kwa wanachama
wa CHADEMA.
Katika moja ya picha hizo, Waziri Mkuu Pinda anaonekana akiwa na mlinzi
wake huku akionyesha kadi ya CHADEMA. Hakuna kiongozi yeyote wa CHADEMA
anayeonekana akimkabidhi kadi kama mwanachama mpya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni