UJUMBE KUTOKA NCHI ZA MAZIWA MAKUU WAMTEMBELEA KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, VIJANA , UTAMADUNI NA MICHEZO

JA1 
Katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa maziwa makuu ambao upo nchini ukiangalia ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu wa Tanzania.Wengine kwenye picha ni Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya katika wizara ya mambo ya nje,Muburi Muita(wa kwanza Kushoto waliokaa) na Nancy kaizilege wa Umoja wa mataifa Tanzania.(wa kwanza kulia waliokaa).

JA2 
Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya katika wizara ya mambo ya nje,Muburi Muita(aliyenyoosha mikono) akiongea na Katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati alipomtembelea ofisini kwake na ujumbe wa kutoka eneo la maziwa makuu(ICGLR) waliokuja kuangalia ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu wa Tanzania na kuelezea kufurahishwa na ushiriki wa vijana wengi katika uchaguzi huu na kwamba uchaguzi ulikuwa wa Amani na mafanikio makubwa.Ujumbe huo unajumuisha nchi za Zambia,Burundi,Kenya,Congo,Uganda na Sudan

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni