Waasi wenye kufuata mrengo wa
kushoto nchini Colombia wamevamia kundi lililokuwa limebeba kura na
kuuwa watu 12, vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimeeleza.
Waziri wa Ulinzi Luis Carlos
Villegas amesema kundi hilo la mrengo wa kushoto katika eneo la
kaskazini mwa Guican, lilifanya shambulio hilo.
Amesema kundi la Jeshi la Taifa la
Ukombozi wa Colombia ambalo ni kundi kubwa la waasi nchini humo ndilo
lililotekeleza shambulizi hilo. Rais Juan Manuel Santos ameahidi
kujibu mapigo ya tukio hilo dhidi ya waasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni