
Rais wa Syria 
Bashar al-Assad amefanya mashauriano na Rais wa Urusi Vladimir Putin 
baada yake kufanya ziara ya kushtukiza Moscow.
Msemaji wa Rais wa 
Urusi Dmitry Peskov amesema Assad "alikuwa kwenye ziara ya kikazi 
Moscow" Jumanne na alifanya mazungumzo na Bw Putin.
Mwishoni mwa 
mwezi jana, ndege za kijeshi za Urusi zilianza kushambulia maeneo 
yanayodhibitiwa na wapinzani wa Assad nchini Syria.
Urusi imejitetea na kusema inashambulia tu makundi ya kigaidi na wapiganaji wa Islamic State.
Bw Peskov ameambia wanahabari kwamba viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu viva hivyo alivyosema ni dhidi ya magaidi.
Aidha,
 walizungumzia kuendelea kwa mashambulio ya ndege za Urusi na mpango wa 
Syria kuhusu wanajeshi. Haijabainika iwapo Bw Assad bado yuko Moscow au 
amerejea Damascus.
Hiyo ndiyo ziara ya kwanza kabisa kufanywa na 
Bw Assad nje ya nchi tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe 
nchini Syria 2011, runinga ya serikali nchini Syria imesema.
Taarifa
 kuhusu mazungumzo hayo iliyotolewa na Kremlin inaonyesha Bw Putin 
akieleza Syria kama “rafiki” na kusema Urusi iko tayari kuchangia “sio 
tu kijeshi…bali pia katika mchakato wa kisiasa” kurejesha Amani nchini 
humo.
 
 
 
 
  
 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni