Kiongozi mmoja mkubwa wa waasi Sudan
Kusini ameiambia BBC huenda wakachukua silaha tena na kupambana licha
ya kusaini makubaliano ya amani wiki sita zilizopita.
Jenerali Johnson Oloni amesema
serikali imekuwa ikikiuka makubaliano hayo kwa kushambulia raia na
inapanga kuweka mipaka mipya katika taifa hilo.
Makumi kwa maelfu ya watu wamekufa
na mamilioni wameachwa bila ya makazi tangu kuibuka mapigano ya
wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.
Nchi ya Sudani Kusini imepata uhuru
wake kutoka kwa nchi ya jirani ya Sudani miaka minne iliyopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni