Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la
Nyamagana Mkoani Mwanza ameibuka mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumbwaga aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata kura 79,280.

Matokeo
hayo yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimboni humo ambae pia
ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito Mahinya huku kukiwa na Ulinzi
Mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama katika viunga vya ofisi za Jiji
hilo.
Akitakangaza
matokeo hayo majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Mahinya
alibainisha kuwa pia CCM imeibuka kidedea kwa upande wa Madiwani ambapo
kati ya Kata 18, imeshinda Kata 14 na Chadema Kata Nne.Kwa upande wa
Wagombea wengine, Chacha Okong’o (ACT Wazalendo) alipata kura 161, Faida
Potea (CUF) amepata kura 1,005, Ahmad Mkangwa (NRA) kura 104, Mohamed
Msanya (Jahazi Asilia) kura 175 na Ramadhan Mtoro (UDP) amepata kura 68.
Hata
hivyo kabla ya matokeo hayo kutangzwa, Mgombea kutoka Chadema Ezekiel
Wenje alikataa kusaini karatasi ya wagombea na kubainisha
kuwa demokrasia haikutumika katika zoezi zima la uhesabuji wa kura katika
uchaguzi huo na kwamba atafuata hatua zaidi za kisheria katika kupinga matokeo hayo.
kuwa demokrasia haikutumika katika zoezi zima la uhesabuji wa kura katika
uchaguzi huo na kwamba atafuata hatua zaidi za kisheria katika kupinga matokeo hayo.
Kwa
upande wake Mshindi wa Uchaguzi huo Stanslaus Mabula alisema kuwa tangu
awali alitarajia ushindi huo na kwamba sualala demokrasia
limezingatiwa.
Katika hatua nyingine Mabula alibainisha kuwa
atahakikisha anatatua changamoto zinazolikabili Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wakazi wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili waweze kujitegemea kiuchumi.
atahakikisha anatatua changamoto zinazolikabili Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wakazi wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili waweze kujitegemea kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni