Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia)
akizungumza na uongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma
alipofanya ziara wilayani humo kwa ajili ya kukagua Kambi ya Nduta
wilayani humo pamoja na Kambi za Mtendeli na Karago wilayani Kakonko
ambazo zipo katika maandalizi ya kuwapokea wakimbizi wa Burundi
wanaohifadhiwa kwa muda katika Kambi ya Nyarugusu mkaoni humo. Katikati
ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
Mhandisi
wa Maji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
Msafiri Mtyaule akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) kuhusu kisima ambacho
kitasambaza maji kwa ajili ya wakimbizi kutoka Burundi ambao
watahifadhiwa katika Kambi ya Mtendeli wakitokea Kambi ya Nyarugusu
ambapo wanahifadhiwa kwa muda.
Mkuu
wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Fred Nisajile akimuonyesha Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili
kulia) moja wapo ya madarasa yatakayotumiwa na wakimbizi
watakaohamishiwa katika Kambi ya Karago kutoka Kambi ya Nyarugusu
wanapohifadhiwa kwa muda. Ubaoni ni picha na maandishi yaliyoachwa na
wakimbizi walioishi katika kambi hiyo kabla ya kufungwa mwaka 2007.
Baadhi
ya Wakimbizi kutoka Burundi wakipokelewa katika Kambi ya Wakimbizi ya
Nduta. Idadi ya wakimbizi kutoka nchini humo inazidi kuongezeka siku
hadi siku.
Askari
Polisi wanaosimamia usalama katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta
wakikagua mizigo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaopokelewa katika kambi
hiyo ili kuhakikisha usalama wa mizigo yao.
Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambapo wanahifadhiwa.
Baadhi
ya mahema yanayojengwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani
Kibondo mkoani Kigoma ambayo yatatumika kuwahifadhi wakimbizi kutoka
Burundi wanaoendelea kuwahamishiwa kambini hapo kutoka Kambi ya
Nyarugusu ambapo walikuwa wamehifadhiwa kwa muda.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni