Muangalizi Mkuu wa EU EOM, Judith Sargentini, Mbunge wa Bunge la Ulaya akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) nchini.Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya
Tanzania – Uchaguzi Mkuu 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Date: 27/10/2015
Ya kutolewa mara moja
Uchaguzi uliyokuwa na ushindani mkubwa, uliyopangwa vyema kwa kiasi kikubwa,
lakini ambao haukuwa na jitihada za kutosha za uwazi toka kwa watendaji wa uchaguzi
Dar es Salaam, 27 Oktoba 2015
Uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba ulikuwa na ushindani mkubwa, kwa kiasi kikubwa
umeendeshwa vizuri, japokuwa jitihada pungufu za uwazi zilimaanisha kuwa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hazikupewa imani kamili ya vyama
vyote.
Akitoa tamko la awali la ujumbe wa waangalizi Jijini Dar es Salaam, Muangalizi Mkuu wa EU
EOM, Judith Sargentini, Mbunge wa Bunge la Ulaya, alisema japokuwa NEC na ZEC walikuwa
wamejiandaa vyema katika mpangilio wa uchaguzi, kutokuwepo kwa uwazi pamoja na
maelezo kwa wakati kuhusu daftari la wapiga kura, maelezo ya mipaka ya majimbo na mfumo
wa kurusha matokeo kumesababisha kuwepo kwa hisia hasi na kuathiri imani ya vyama juu
ya mchakato wa uchaguzi.
Siku ya uchaguzi ilionekana kuendeshwa vyema. Waangalizi wa EU walifuatilia taratibu za
upigaji kura kwenye vituo 625 katika mikoa yote nchini. Uendeshaji wa upigaji kura
ulionekana kwenda vyema katika asilimia 96 ya vituo vya kupiga kura vilivyoangaliwa na EU
EOM, kwa Tanzania bara na Zanzibar. Wawakilishi wa vyama vya siasa walikuwepo kwenye
karibia vituo vyote vilivyoangaliwa, jambo ambalo lilichangia kuwepo kwa uwazi na imani juu
ya mchakato wa upigaji kura. Tathmini ya jumla ya ufungaji pamoja na utaratibu wa kuhesabu
pia ilionekana kuwa nzuri au nzuri sana katika vituo vilivyo vingi vilivyoangaliwa.
“EU ilikuwa na waangalizi 141 kwenye mikoa yote ya Tanzania siku ya uchaguzi,” alisema Bi
Sargentini. “Japokuwa kulikuwa na matatizo madogo madogo kwenye vituo vichache vya
kupiga kura, kilichoonekana kwa ujumla ni mamilioni ya watu wakitumia haki yao ya kupiga
kura katika mazingira ya amani, na wakionyesha dhamira yao ya kuunga mkono mchakato wa
kidemokrasia.”
Bi Sargentini alisema kuwa waangalizi wa EU walihudhuria zaidi ya shughuli 139 za kampeni
nchini kote. Pamoja na mabishano kadhaa kati ya mashabiki wa vyama vinavyopingana,
baadhi ambayo kwa kusikitisha yaliishia kwa vurugu, alisema kuwa, kwa ujumla, kampeni
zilikuwa safi na za kusisimua.
Kuhusu mifumo ya kisheria, EU EOM imesema kuwa, pamoja na kuwa mifumo inayotawala
chaguzi kwa Muungano na Zanzibar inatoa msingi mzuri wa uendeshaji wa chaguzi za
kidemokrasia, kuna maswala kadhaa ambayo hayajafanyiwa kazi toka uchaguzi uliyopita.
Haya ni pamoja na kutoruhusiwa kikatiba kwa wagombea binafsi na kutokuweza kupinga
matokeo ya uchaguzi wa rais, ambayo hayaendani na misimamo ya kimataifa kwa chaguzi za
kidemokrasia.
EU EOM iliangalia vituo vya habari 16 wakati wa kampeni. Ili baini kuwa vyombo vya habari
vya dola havikutoa nafasi sawa na za haki za habari za kampeni, huku CCM ikipewa nafasi
zaidi. Hata hivyo katika mtazamo chanya, Bi Sargentini alisema kuwa baadhi ya vyombo vya
habari binafsi vilionekana kwa kiasi kikubwa kutoa uwiano.
Waangalizi wa EU watabaki nchini kufuatilia mchakato wa uorodheshwaji na utangazaji wa
matokeo, na malalamiko na rufaa zinazoweza kujitokeza.
“EU EOM itabaki nchini hadi tarehe 15 Novemba, na itakutana na vyama, maafisa uchaguzi na
asasi za kiraia,” alisema Bi Sargentini. “Kwa ajili ya wapiga kura wote waliyopanga foleni kwa
subira Jumapili, natumai ya kuwa wahusika wote wataendelea kufanya kazi ili kuwa na
chaguzi za amani, shirikishi na zenye uwazi.”
“Hitimisho la amani la uchaguzi pamoja na dhamira ya kuimarisha demokrasia ya vyama vingi
vitahakikisha historia ya kujivunia ya Tanzania ya uongozi, kikanda na barani,” alisema Ines
Ayala Sender, Mkuu wa Wawakilishi wa Bunge la Ulaya, ambao walijiunga na Ujumbe wa
Waangalizi wa EU siku chache kabla ya siku ya uchaguzi. “Hivyo basi, nawahimiza Watanzania
wote kuwekea mkazo maisha ya kisiasa shirikishi, ujengaji imani na uaminifu, na uimarishaji
zaidi wa taasisi zinazo unga mkono demokrasia.”
EU EOM ndiyo ujumbe mkubwa kabisa wa waangalizi wa kimataifa uliyopo nchini na ambao
upo Tanzania kwa muda mrefu zaidi. Ilitathmini ni kwa kiasi gani mchakato wa uchaguzi
ulifuata ahadi za kimataifa na za kikanda kuhusiana na chaguzi, pamoja na sheria za Tanzania.
EU EOM itatoa tamko kamili lenye maelezo ya kina ikiwa ni pamoja na mapendekezo kwa
chaguzi zijazo, katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya kukamilika kwa mchakato wa
uchaguzi.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Sarah Fradgley, Afisa Habari EU EOM Simu ya mkononi: +255 786 440768 Barua pepe: sarah.fradgley@eueomtanzania.eu
Tovuti: www.eueom.eu/tanzania2015 Facebook: www.facebook.com/eueomtanzania2015 Twitter: @EUEOMTanzania

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni