CHADEMA WAONGOZA JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI KWA ASILIMIA 73



 mkurugenzi wa uchaguzi akiwa anatangaza matokeo ya
ubunge na urais  wa jimbo la arumeru magharikibi

 picha ikionyesha wananchi  na waandishi wa habari wakiwa wanaangalia
matokeo ya ubunge na urais yaliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo
katika jimbo la Arumeru magharib

 mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru magharibi akiwa
makini kusikiliza matokeo ya urais na ubunge ya jimbo lake wakati
mkurugenzi wa  halmashauri ya  meru ambaye pia msimamizi wa uchaguzi
wa jimbo  hilo Fidelis Lumato
Na Mahmoud Ahmad

Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Olemeiseyeki Gibson  Blasius  amewashukuru wananchi wa jimbo lake kwakuweza kumchagua kuongoza jimbo hilo  na amewahidi kutofanya mchezo katika kipindi cha uongozi wake.


Ameyasema hayo leo mara baada ya kutangazwa  kuwa mshindi wa jimbo hilo baada yakuongoza   kwa kura nyingi zaidi ya wenzake.


Alisema kuwa anawashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura nakumchagua kwani hii wamemuona ni kiongozi  anaeyefaa kuwaongoza na ni kiongozi mchapakazi.

Adha aliwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kuweza kumpa madiwani wengi zaidi  katika halmashauri yake na kusema kuwa  kati ya kata 27 zilizopo jimboni kwake  jumla ya kata 21 ni za chadema  na zingine 6 niza CCM


Kwa mujibu  wa taarifa iliyotolewa  na mkurugenzi wa Halmashauri  ya meru ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Arumeru magharibi wakati akitangaza matokeo  matokeo ya nafasi ya urasi katika jimbo hilo Fidelis Lumato  alianza na chama cha Act ambapo waliweza kupata kura 324  ,ADC 250 ,CCM27658,CDM 105720,CHAUMA 388,NRA58,TLP54 pamoja na UPDP 40.

Kwa upande  wa jimbo la Arumeru magharibi  mgombea huyu wa ubunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Olemeiseyeki Gibson  Blasius  ameweza kuongoza  kwa asilimia 73% ambapo alipata  kura 94354  huku mgombea aliyemfuata ni wa chama cha mapinduzi( CCM)Sabaya  Loy Thomas  ambaye alipata kwa asilimia 25%  ambapo alipata kura 32831 huku chama cha ACT Wilson Loilole Laizer kikiwa kimepata kura kwa asilimia 2% ambapo walipata kura 2457.

Lumato alisema kuwa anapenda kuwashukuru wananchi pamoja na wagombea kwa jinsi walivyoonyesha  hali ya utulivu katika kipindi chote cha kampeni pamoja,upiga kura pamoja na kupokea matokeo na amewaomba waendelee hivyo hivyo hata katika chaguzi zijazo.


Afafanua kwanini wamechelewa kutaja matokeo na kusema kuwa hii imetokana na tatizo la mtandao ambapo lilitokea tangu hali iliyowapelekea  kuchelewesha matokeo hadi leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni