WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAAJIRI WATUMISHI WAPYA 588

2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na waajiriwa wapya katika Ufunguzi wa Semina Elekezi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara Rasilimali watu Bw. Said Msambachi ( wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu Bi. Aurelia Matagi , ( wa kwanza kushoto) , Kwa upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Zahoro Kimwaga pamoja Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keryaro.
3
Baadhi ya Watumishi wapya walioajiriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika Ufunguzi wa Semina Elekezi ya Waajiriwa wapya iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.
4
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu Bi Aurelia Matagi ( kulia) akiwa na Afisa Utumishi Mwandamizi Bw. Safari, wakiwa wanatoa maelekezo ya kujaza fomu za kuajiriwa katika Semina Elekezi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.
1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keryaro ( kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali watu Bw. Said Msambachi ( kulia) mara baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Meru kuwasili katika ufunguzi wa Semina Elekezi ya waajiriwa wapya iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.



                                                                                               Na Mwandishi wetu

Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa ajira mpya kwa Watumishi wapya wapatao 588 ikiwa idadi kubwa miongoni mwao ni Watumishi wa kada ya Afisa Wanyamapori na Wahifadhi wanyamapori lengo likiwa ni kukabiliana na mashambulio mengi kutoka kwa majangili.
 

Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo elekezi kwa waajiliwa wapya hao yaliyofanyika leo katika Chuo cha Taifa cha Utalii katika Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Dkt. 

Adelhelm Meru amesema watumishi hao ni lazima wajitume ili kukidhi malengo kwa kudhibiti na kusimamamia matumizi endelevu ya wanyamapori pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira ya mapori ya akiba.
 

‘’Fursa hii mliyoipata isaidie kuongeza chachu na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa kuhakikisha kuwa Maliasili tulizonazo zinalindwa na kutunzwa kikamilifu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye’’ Dkt. Meru alisisitiza.
 

Amewataka watumishi hao kufanya doria katika maeneo ya mapori ili kuimarisha uwepo wa Wanyamapori katika maeneo ambayo Watalii wanaweza kupata fursa ya kuwaona kwa urahisi zaidi.
 

Aliongeza kuwa Watumishi hao ni lazima waweke nguvu na mikakati endelevu katika kupambana na uchomaji moto ovyo wa mapori, kilimo na uingizaji wa mifugo katika maeneo ya mapori yaliyotengwa kwa ajili ya Wanyamapori
 

Pia aliwataka Watumishi hao kujiepusha na na tabia ya kupokea rushwa hasa kwa watumishi walio kwenye Mapori ya akiba, mapori tengefu na vituo vingine vya kazi na Mtumishi yeyote atakayethibitika kupokea rushwa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupoteza ajira yake.
 

Aidha, Dkt. Meru amewaasa watumishi wapya kujiepusha na anasa na ulevi wa kupindukia likiwemo janga la Ukimwi ambalo limekuwa sio rafiki kwa nguvu kazi ya taifa ambayo imepatikana kwa gharama kubwa
 

Watumishi wapya wapatao 588 walioajiriwa ni Maafisa wanyamapori daraja la pili 111, Maafisa Utalii daraja la pili 17, Wahifadhi wanyamapori daraja la pili 14, Wahifadhi Wanyamapori la pili tatu 433.

Wengine ni Wahasibu wasaidizi 11, Msaidizi wa Maktaba 1 na fundi sanifu Umeme 1, Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tatu.
 

katika idara mbalimbali wakiwemo, wahifadhi wa wanyamapori daraja la (2) 14, wahifadhi wanyamapori daraja la (3) 433 uhasibu wasaidizi 11, fundi umeme 1, maofisa utalii daraja la (2) 17, msaidizi wa Maktaba 1, leo Asubuhi katika ghafla ya kuwa karibisha na kuwapa mafunzo waajiliwa hao iliyofanyika jijini Dar es salaam katika chuo cha utalii kilichopo Temeke. Dkt. 

Meru alisema, rushwa ni tatizo kubwa katika Taifa letu hivyo Wizara ya Maliasili na Utalii haina budi kuwa mfano wa kuigwa katika kupiga vita rushwa na kutatua matatizo ya wafanyakazi hasa kwa watumishi walio kwenye Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na vituo vingine vya kazi.

Pia aliongezea nakusema, napenda nimalizie kwa kuzumzia kwa kifupi tatizo lingine linalokabili Taifa letu, Tatizo hili ni janga la ukimwi. Uboreshaji wa utendaji kazi katika utumishi wa Umma hususani ulinzi wa Wanyamapori hauwezi kufanikiwa ikiwa janga la Ukimwi halitadhibitiwa. 


UKIMWI unasababisha vifo vya watumishi hivyo kulipunguzia Taifa nguvu kazi ambayo imepatikana kwa gharama kubwa, kwa hiyo kila mmoja wenu anatakiwa ashiriki kikamilifu katika kujikinga na janga hilo na kuchukua tahadhari kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. 

Wizara itaendelea na jukumu lake la kuelimisha wafanyakazi kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI.
 

Pia mmoja wa waajiliwa hao nae alimshukuru katikbu Mkuu kwaniaba ya waajiliwa wenzake na kuahidi kuwa watafanya kazi kikamilifu, watakuwa waadilifu na watashirikiana na wafanyakazi wengine wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni