Baadhi
 ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya 
kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani 
Kilimanjaro.
Na Mwandishi wetu
TAASISI
 ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili  mradi wa kituo 
cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha 
upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.
Imeelezwa
 kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 
kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo 
la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.
Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani  na kijiji hicho.
Ufadhili
 huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa 
wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha
 ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.
Taasisi
 ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya 
MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha 
Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa 
wakufadhili mkoani Singida.
Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.
Toka
 mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya 
urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. 
Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya 
dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
Baadhi
 ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la 
kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada
 wa Mo Dewji Foundation.
Tangu
 kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na 
kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa 
visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi
 waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi 
wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho
 katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa
 waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa
 vya wakulima.
Kwa
 mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, 
wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa 
ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.
Alisema
 wazo la kuanzishwa kwa  kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya 
mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.
 “Elimu
 imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali 
ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika
 wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila 
kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na  bayolojia,” alisema Isiaka
 na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo 
kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.
“Tunaamini
 kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi
 vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.
Kwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.
 “Kwa
 kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia  ya maktaba na tehama, wanafunzi
 wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya 
kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.
Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.
Kituo
 cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka 
katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani
 Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha 
Kisangara.
Kijiji
 cha Kisangara  ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa 
kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika 
mashamba ya mkonge.
Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame
 uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya 
umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na 
familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi  na kuwaacha katika shule
 za umma ambazo hazina ubora.
Kutokana
 na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini 
kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw 
aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.
Kituo
 kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa 
kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia, 
kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.
Lengo
 kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma 
shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia 
maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa 
wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.
Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.
Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
Mratibu
 wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia
 matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji 
Foundation.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni