Zaidi ya wastaafu 40 waliokuwa
kwenye safari fupi wamekufa katika ajali ya basi lililogongana na
lori katika barabara kusini mashariki mwa Ufaransa.
Ajali hiyo imetokea karibu na
Puisseguin katika mkoa wa Gironde mashariki mwa Bordeaux, ikiwa si
mbali tangu basi hilo lilipoanza safari yake katika mji uliokaribu.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
ametuma twitti akisema serikali imeguswa mno na tukio hilo la ajali
hiyo mbaya.
Hii ni ajali mbaya ya barabarani
kutokea nchini Ufaransa tangu mwaka 1982 ambayo iliuwa watu 52.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni