Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Pichani) amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya shughuli ya kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu kitaifa kwa upande wa Chama hicho inayotarajiwa kufanyika hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba yamekamilika.
Na:George Binagi-GB
Pazzo kubwa
itafungwa nje ya uwanja huo kwa ajili ya wale watakaokosa nafasi ya
kuingia uwanjani kwa kuwa shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na
maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na Maeneo jirani.
Mbali na
Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli kuwepo katika mkutano huo,
pia Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anaemaliza muda wake Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa miongoni
mwa viongozi watakaohudhuria katika Mkutano huo wa Ufungaji wa Kampeni
za Uchaguzi Mkuu kwa upande wa CCM.
Wakati
Watanzania wakitarajia kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu siku ya kesho
jumapili ya Octoba 25, Chama cha Mapinduzi CCM kimejihakikishia ushindi
mnono katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge
na Urais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni