Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla ( katikati ) akiwa na viongozi wakuu wa jeshi la polisi mkoani humo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akizungumza na maofisa mbalimbali wa jeshi la polisi mkoani humo.
Mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla amezungumza na polisi wa Manispaa
ya Moshi na kuwataka wahakikishe uchaguzi unafanyika kwa amani na
utulivu ili kila Mwananchi apate haki ya kupiga kura bila kubughudhiwa.
Amewataka polisi kuhakikisha kuanzia sasa, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi wahakikishe amani inatawala na katika kutekeleza majukumu yao wazingatie maadili ya polisi.
Aidha akiwa katika gereza la Karanga, mkuu huyo wa mkoa wa Kilimanjaro amekagua malazi ya wafungwa na mahabusu, na baadaye akaongea na baraza la Askari na kukagua kiwanda cha viatu na ushonaji unaofanywa na wafungwa na mahabusu
Amepongeza ubora wa viatu vinavyotengenezwa kiwandani hapo na bidhaa za ushonaji unaofanywa na gereza ka wanawake
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akisalimiana na maofisa wa jeshi la Magereza alipotembelea gereza la Kuu la Karanga lililopo nje kidogo ya mji wa Moshi.
Maofisa wa jeshi la Magreza wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla ( hayupo pichani ) wakati alipokutana na kuzungumza nao.
Maofisa wa Magereza wakimtembeza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla ( mwenye kaunda suti ya kaki ) alipotembelea gereza kuu la Karanga lililopo nje kidogo ya mji wa Moshi.
Picha ya pamoja
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akikagua viatu vinavyotengenezwa na wafungwa wanaotumikia vifungo vyao katika gereza kuu la Karanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni