Jitihada za uokoaji zinaimarika
kusaidia watu walioathirika na tetemeko lenye kipimo cha alama 7.5
lililolikumba eneo la kando la Afghanistan na Pakistan hapo jana.
Watu wapatao 275 inasemekana
wamekufa na zaidi ya 2,000 wamejeruhiwa. Timu ya uokoaji imetumwa
katika mlima ulio eneo le kando ambako madhara ya tetemeko
hayajajulikana.
Miongoni mwa waliopoteza maisha ni
pamoja na wanafunzi wa kike nchini Afghanistan ambao walikufa kwa
kukanyagana wakati wakijaribu kutoka kwenye jengo lililoanguka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni