WANAFUNZI 13 WA CHUO CHA LIMPOPO NJE YA MJI WA POLOKWANE WASHIKILIWA AFRIKA KUSINI

Wanafunzi 13 wa chuo cha Limpopo nje ya mji wa Polokwane nchini Afrika Kusini wamekamatwa kwa kuharibu kwa makusudi majengo pamoja na kuiba, wakati wakipinga ongezeko la ada.

Wanafunzi hao waliokuwa wakiandamana waliharibu jengo la mgahawa katika kampasi ya Turfloop hapo jana usiku.

Tukio hilo limetokea saa chache baada ya kuwasilisha waraka wao kwa uongozi wa chuo, kuelezea maandamano yao hayo ambayo ni sehemu ya maandamano ya kitaifa Afrika Kusini kushinikiza kushushwa kwa ada. 
Wanafunzi hao walipambana na polisi katika ghasia hizo usiku mzima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni