Kijana aliyefunika uso wake ambaye
alimuua mwalimu na mwanafunzi katika shule nchini Sweden, alisukumwa
na dhamira ya ubaguzi.
Mkuu wa polisi Niclas Hallgren
amesema wamebaini hilo baada ya kukuta ushahidi kwenye makazi ya
muuaji huyo, unaoelezea mwenendo wa matendo yake.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa
kijana huyo mwenye umri wa miaka 21, alikuwa ni mfuasi wa kundi lenye
kufuata msimamo wa mrengo wa kulia.
Kijana huyo aliyekuwa amevaa kofia
ya pikipiki na kufunika uso wake akiwa na jambia alivamia shule hiyo
eneo la Trollhattan karibu na Gothenburg, kabla ya kupigwa risasi na
kufa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni