Polisi nchini Mexico wamebaini njia
ya shimo la aridhini yenye urefu wa mita 800, inayotumika
kusafirishia dawa za kulevya kwenda Mji wa San Diego nchini Marekani.
Shimo hilo linaloanzia katika mji wa
Tijuana nchini Mexico, linasemekana ni la mkuu wa genge la dawa za
kulevya anayetafutwa Joaquin Guzman.
Polisi nchini Mexico wamesema
wanawashikilia watu 16, na wamekamata tani 10 za bangi.
Wauza dawa za kulevya nchini Mexico
wamekuwa wakisafirishwa kwa njia za magendo dawa za kulevya kwenda
Marekani kupitia njia za mashimo ya aridhini.
Polisi akilinda shehena ya dawa za kulevya iliyokamatwa
You might also like:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni