Nyota wa filamu Angelina Jolie licha
ya kuwa miongoni mwa nyota wakubwa kabisa duniani lakini anapenda
kuishi maisha ya kawaida badala ya yale ya udiva.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 40,
ameonekana akiwasili katika uwanja wa ndege wa LAX akivuta mwenywe
begi lake la matairi bila ya kuwa na msaidizi kama wafanyavyo mastaa
wengine, akiwa na watoto wake.
Angelina Jolie alikuwa na watoto
wake hao Maddox, Pax, Zahara pamoja na Shiloh, ambao nao walikuwa
wamebeba mabegi yao mgongoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni