Chama cha Conservative cha Sheria na
Haki kimeshinda uchaguzi wa bunge nchini Poland.
Kura za mwisho zinaonyesha chama
hicho kimepata viti vingi kuweza kutawala peke yake, huku ikitarajiwa
kupata kura asilimia 39.
Kiongozi wao Jaroslaw Kaczynski
amedaia kupata ushindi, huku waziri mkuu anayeondoka Ewa Kopacz wa
chama cha mrengo wa kati cha Civic Platform akikubali kushindwa.
Chama cha Sheria na haki kinaungwa
mkono mno katika maeneo ya vijijini nchini Poland.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni