WANANCHI PIGENI KURA KWA AMANI NA UTULIVU ,EPUKENI MAKUNDI YASIO RASMI

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas akiwa anaongea na waandishi wa habari hii leo kuhusiana na hali halisi ya usalama katika siku ya kupiga kura hapo kesho
 waandishi wa habari wakiwa wanamsikiliza kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha (hayupo pichani) wakati alivyokuwa na mkutano na wandishi wa habari ndani ya makao makuu ya polisi mkoani hapa

Na Woinde Shizza,Arusha

Kamanada wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amewataka wananchi wanahakikisha uchaguzi unaenda kwa amani na utulivu na watambue wanawajibu wa kuilinda amani yao na pia kutii sheria  bila shuruti .

Hayo ameyasema leo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake huku akiwataka wananchi kufuata maagizo  yanayotolewa viongozi kuhusu swala zima la kulinda amani yao na kufanya uchaguzi wa utulivu bila ya kuvuruga amani ya nchini.
 Alisema kuwa  katika kipindi kizima cha kampeni zimeenda kwa amani na utulivu japo kuna mambo yalitokea katika kati lakini ni ya kawaida na sio makubwa ,hivyo amani iliyokuwepo katika kipindi hicho cha kampeni idumishwe hata katika kipindi cha uchaguzi  na kila mwananchi ajitokeze kwenda kupiga kura maana kura yake ndio itampa mustakabali  taifa letu  katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aliongeza kuwa kila mwananchi ni mdau wa kuakikisha uchaguzi unaenda kwa amani na utulivu na sio kwa kuwategemea polisi katika kulinda amani ya nchi kwani wote ni wadau wa kuilinda amani ya nchi

Aidha alitoa angalizo kuwa  katika siku hii  ya uchaguzi airuhusiwi mwananachi yeyote kusimama katika makundi ya watu wawili wawili wakidai wanasubiri kulinda kura  ,kwani kura italindwa na waliopewa dhamana .
Akabinisha kuwa ukisha piga kura unatakiwa kurudi kwako  au kwenda kuendelea na shughuli zako na sio kuka katika makundi ambayo yanaviashiria vya  kuvunja amani na kuaribu uchaguzi.

"jeshi la polisi limepata taarifa kuwa kuna baadhi  ya vyama ambavyo vimeandaa jeshi kwa ajili ya vurugu  na kuwapa mafunzo  kwa ajili ya kuleta fujo wakati wa uchaguzi ,na wametageti katika baadhi ya maeneo wanayo yajua sasa nasema tumewagundua na nawashauri wabaki majumbani mwao kwani wakifanya hivyo jeshi letu la polisi alita wafumbia macho"alisema Sabas


Aliwataka wananachi wakishapiga kura kuendelea na shughuli zao za  ujenzi wa taifa na kuwa swala la ulinzi na usalama  ni la vyombo vya usalama na sio la raia  wala makundi ya vyama .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni