Kampuni kubwa ya simu ya MTN nchini
Nigeria imepigwa faini iliyoweka rekodi ya dola bilioni 5.2 na Tume
ya Mawasiliano ya Nigeria (NCC).
MTN wamepigwa faini hiyo kwa
kushindwa kutimiza kwa muda masharti ya NCC ya kuwafutia mawasiliano
watumiaji wa simu ambao hawajasajili kadi zao za simu.
Kampuni ya MTN Nigeria imesema
itapitia barua ya faini hiyo walioyowasilishwa na Tume ya Mawasiliano
ya Nigeria (NCC).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni