MWANZILISHI NA MTENDAJI MKUU WA TWITTA BW. JACK DORSEY KUTOA HISA KWA WAFANYAKAZI

Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa twitta Bw. Jack Dorsey amesema atatoa theluthi ya hisa za kampuni hiyo kwa wafanyakazi wake.

Jumla ya kiasi hicho cha hisa ni asilimia 1 ya kampuni sawa na dola milioni 197.

Bw. Dorsey amesema kampuni yake itawekeza moja kwa moja katika watu wake. Wiki iliyopita kampuni ya twitta ilisema itapunguza wafanyakazi 336 ama asilimia 8 ya wafanyakazi wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni