NYUMBA
ya Naibu sheha wa shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba,
Bikombo Simai Juma (42), ambayo imedaiwa kuchomwa moto na watu
wasiofahamika kwa madai ya hitilafu za kisiasa, tukio hilo lilitokea
oktoba 26, majira ya saa 7:00 usiku, ambapo wakati huo alikuwa ndani
amelala na jumla ya watu 13 akiwemo mtoto mchanga wa mwezi mmoja,
walisalimika kufa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
NYUMBA
nyengine ilioko kando mwa nyumba ya naibu sheha, eneo hilo la
Tibirinzi, kijiji cha Minazini, ikiwa imechomwa moto nyuma kwenye eneo
la choo cha makuti, inayomilikiwa na Khamis Kassim Juma siku hiyo hiyo
ya Oktoba 26 usiku wa saa 7:00 ambapo matukio yote hayo hakuna
aliejeruhiwa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
NAIBU
sheha wa shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba Bikombo Simai
Juma (24) akizungumza na mwandishi wa habari hizi hayupo pichani, muda
mfupi baada ya nyumba yake kudai kutiliwa moto na watu wasiofahamika,
(Picha na Haji Nassor, Pemba). Kwa hisani ya ZanziNews
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni