Nchi ya Congo-Brazzaville inafanya
upigaji kura ya maoni kuhusiana na kubadilishwa Katiba katika
kumruhusu rais Denis Sassou Nguesso kugombea kwa muhula wa tatu.
Viongozi wa upinzani wametaka
kususiwa kwa kura hiyo baada ya idadi kadhaa ya waandamanaji kupigana
na maafisa wa ulinzi.
Chini ya Katiba ya sasa, rais
Nguesso hawezi kuwania urais kutokana na kuwa na umri zaidi ya miaka
70, na tayari ametumikia mihula miwili. Rais Sassou Nguesso aliingia
madarakani mwaka 1979.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni