SAED KUBENEA AIBUKA MSHINDI WA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO

                                                       Said Kubenea ( kushoto ). Picha kutoka maktaba

Mwandishi mahiri wa habari nchini, Saed Kubenea ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam. 

Matokeo hayo yemetangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ubungo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty.

Akitangaza matokeo hayo, Mhandisi Natty amesema Said Kubenea amepata jumla ya kura 87,666 huku mpinzani wake wa karibu mgombea wa Chama Cha Mapinduzi, Mh Didas Masaburi akipata kura 59,514.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni