Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha 
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Ifuatayo ni taarifa aliyoisoma masaa machache yaliyopita katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Ndugu waandishi wa habari;
Tumewaita
 hapa kuwaomba muwaeleze Watanzania wenzetu, jumuiya ya kimataifa na 
marafiki zetu wengine wa ndani na nje, kwamba hatukubaliani na matokeo 
ya uchaguzi mkuu wa rais, yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya 
Uchaguzi (NEC), kote nchini.
Hii
 ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa
 matokeo hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa 
kusaidiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika
 maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa
 kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa 
halisi ya wananchi.
Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli.
Katika
 baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa 
mgombea wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na 
idadi halisi ya kura zilizopigwa.
Kwa
 mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na 
Mtambile, kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma,
 Same Mashariki, Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni 
miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, 
siyo kura za uchaguzi mkuu wa rais. Tunaweza kuiita, “mzimu wa 
uchaguzi.”
Ndugu waandishi wa habari;
Tangu
 kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda 
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) – mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. 
Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza 
kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya rais,
Hata
 hivyo, Tume imeendelea kutangaza matokeo hayo, bila kujali kile ambacho
 tumekieleza na kukilalamikia, kana kwamba tunachokisema ni ujinga, 
uzushi na uwendawazimu. Hili halikubaliki.
Aidha,
 katika maeneo mengine, likiwamo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyoko 
mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi, yanatofautiana na yale ambayo 
yamekusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo.
Hali
 kama hiyo ipo pia katika majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA na 
wale wa vyama washirika vya CUF na NCCR – Mageuzi, ama wamekuwa na nguvu
 kubwa au wameibuka washindi.
Upo
 ushahidi wa wazi ambao, ninyi waandishi mnaweza kwa kutumia uandishi 
wenu kuuthibitisha kwamba, katika majimbo yote ambako wagombea wa UKAWA 
wameshinda, TUME imechelea kutangaza matokeo ya urais kwa sababu 
zinazothibitisha kuwapo kwa mikakati ya hila.
Ikumbukwe
 kwamba matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa 
yamekuja baada tu ya Jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya 
kuhesabia kura na kuwakamata wataalam wetu waliokuwa wakipokea matokeo 
ya kura za rais nchi nzima ambayo hadi uvamizi huo ulipofanyika tulikuwa
 tukiongoza katika maeneo mbalimbali.
Ndugu waandishi wa habari;
Tunaamini
 kwa dhati kwamba, uvamizi huo ulifanyika mahususi kwa malengo ya 
kufanikisha uchakachuaji huo ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika 
kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa sasa na NEC.
Wakati
 tukijua kwamba NEC ndiyo mamlaka pekee ya kisheria ya kutangaza matokeo
 ya urais, tunapenda kuwataarifu Watanzania na jumuiya ya kimataifa 
kwamba hadi wakati uvamizi huo ulipofanyika kura zetu za urais 
tulizokuwa tumezikusanya zilikuwa zikionyesha tukiongoza kwa asilimia 
zaidi ya 60.
Kutokana
 na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na watendaji wa NEC,
 mimi Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano na 
Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, tunautangazia umma wa Watanzania na 
Jumuiya ya Kimataifa, kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na 
NEC.
Ndugu waandishi wa habari;
Kutokana
 na makosa hayo makubwa, tunaitaka NEC kusitisha mara moja utangazaji wa
 matokeo ya urais na kuanza upya kufanya uhakiki wa kile wanacholetewa 
na wasimamizi wa majimbo ambacho ushahidi unaonyesha kuwapo kwa vitendo 
vya hila ambavyo vinafanywa na NEC.
Ndugu wana habari
Kile
 kinachofanywa na NEC hapa ndiyo kile kile kinachoendelea kufanywa kule 
Zanzibar leo na ZEC ambako kunafanyika juhudi kubwa na za makusudi 
kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa wazi wa ushindi wa Mgombea 
urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni