Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndugu Yahaya Nawanda baada ya kuwasili kwenye
eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi Mjini
kwenye sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo tarehe 11.10.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Bwana Ibrahim Sharaf, Rais wa Sharaf
Group of Companies ya nchini Dubai mara baada ya kuwasili kwenye Shule
ya Sekonadi ya Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi. Rais Kikwete alikuwa
mgeni rasmi katika sherehe ya uzinduzi wa Shule hiyo tarehe 11.10.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiondoa kitambaa kwa kushirikiana na Bwana Ibrahim
Sharaf aliyefadhili ujenzi wa Shule ya Wasichana ya WAMA Sharaf ikiwa
ni ishara ya kuizindua rasmi. Baadaye Rais Dkt. Kikwete akishirikiana na
viongozi wengine walisaidia ujenzi wa shule hiyo kukata utepe ikiwa ni
mwendelezo wa sherehe za ufunguzi rasmi wa shule hiyo huko Lindi tarehe
11.10.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwa wamekaa kwenye mojawapo
ya madawati ya wanafunzi na Bwana Ibrahim Sharaf, Mwenyekiti wa Sharaf
Group of Companies (wa kwanza kushoto) na ndugu yake Bwana Sharafuddin
Sharaf ( wa kwanza kulia) wakati wanatembelea sehemu mbalimbali za
shule.
Rais DKT. Jakaya Kikwete akifuatana na Bwana Sharafuddin Sharaf na wageni wengine wakitembelea shule.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete na wageni waalikwa wakiangalia wanafunzi wakifanya
majaribio mbalimbali ya masomo ya sayansi kwenye Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya WAMA Sharaf huko Lindi baada ya kufunguliwa rasmi tarehe
11.10.2015.
Rais
DKT. Jakaya Kikwete na Mama Salma wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi walioshiriki kufanya majaribio ya masomo ya sayansi.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Daud Nassib jinsi wanafunzi
watakavyotumia kompyuta zilizofungwa kwenye shule hii ili kufanikisha
masomo yao.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma wakiwatembeza wageni waalikwa sehemu mbalimbali za shule hiyo.
Baadhi
ya waalikwa kwenye sherehe ya ufunguzi wa Shule ya Sekondari ya
Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi wakifuatilia hotuba mbalimbali
zilizokuwa zikitolewa wakati wa sherehe za ufunguzi wa shule hiyo.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwa viongozi na wageni
waalikwa wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Shule ya WAMA Sharaf
huko Lindi tarehe 11.10.2015.
Mwakilishi
wa Sharaf Group of Companies Bwana Sharafuddin Sharaf akitoa hotuba
yake kwa niaba ya kampuni wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa shule
hiyo iliyojengwa na kampunio yake huko Lindi.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake ya uzinduzi rasmi wa Shule ya
Sekondari ya WAMA Sharaf iliyojengwa na Kampuni Sharaf kutoka Dubai huko
Lindi tarehe 11.10.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akitoa tunzo maalum kwa Kampuni ya Sharaf Group ya
Dubai kwa msaada wao wa kujenga shule hiyo huko Lindi.
PICHA NA JOHN LUKUWI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni