RAIS VLADIMIR PUTIN ATETEA OPERESHENI ZA KIJESHI ZA URUSI NCHINI SYRIA

Rais Vladimir Putin ameitetea Urusi kuhusiana na operesheni zake za kijeshi nchini Syria, amesema lengo lake ni kuipa uhalali mamlaka ya rais wa Syria, Bashar al-Assad.

Rais Putin ameiambia televisheni ya taifa ya Urusi Jijini Moscow pia anataka kujenga mazingira ya kuwepo hali ya maridhano ya kisiasa Syria.

Amekanusha kuwa makombora ya Urusi yanalenga wapiganaji wenye msimamo wa wastani badala ya wapiganaji wa Dola ya Kiislam (IS).

Vikosi vya serikali ya Syria vimesema vimepiga hatua kubwa katika kuwadhibiti waasi wa nchi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni