Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amefanya ziara Chuo cha polisi Moshi ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha na kukagua shughuli mbalimbali katika Chuo hicho chenye uwezo wa kudahili wanafunzi 4,000 kwa wakati mmoja
Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa Chuo ( Commandat CCP) Matanga Mbushi amemweleza mkuu wa mkoa kuwa Chuo hicho kimetoa wanafunzi 2,651 na walimu 115 kushiriki kulinda Raia katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25 October 2015
Akiongea na baraza la Askari Mkuu wa mkoa amekipongeza Chuo hicho kwa kuchangia Askari hao ambao watasambazwa mikoani kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa Amani Na utulivu
Aidha amekupongeza uongozi wa Chuo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kilimo cha migomba, bustani na ufugaji Kuku wa nyama na mayai
Mkuu wa mkoa ameshuhudia Mafunzo ya Askari, kikosi cha mbwa na farasi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni