ZEC YAFUTA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR

Taarifa zilizotufikia kutoka visiwani Zanzibar zinasema kuwa, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kufutwa kwa uchaguzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mpaka hapo itakapotangazwa tena. 
Sababu hasa za kufutwa kwa uchaguzi huo, kunaelezewa kuwa ni kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza. 
Tamko la kufutwa kwa uchaguzi huo limetolewa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alipoongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita huko Zanzibar. 
Na hii ni taarifa kamili iliyosomwa kwa waandishi wa habari na Mwenyeikiti huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni