Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dr Adelhelm Meru akifungua
warsha ya siku moja iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Idara ya
Mambo ya Kale kwaajili ya kujadili uboreshwaji wa utawala na matumizi
endelevu ya hifadhi za urithi na mazingira za Tanzania, ambazo ni Magofu
ya Kilwa; Michoro ya Asili Kondoa; Mji Mkongwe Zanzibar; Hifadhi ya
Wanyama Selous; Hifadhi za Taifa za Serengeti, Ngorongoro, Lake Manyara
na Mlima Kilimanjaro; na Hifadhi ya Mazingira ya Usambara Mashariki’.
Mkuu wa Hifadhi ya Kondoa Rock Art, Zuberi Mabie akichangia mada katika warsha hiyo iliyofanyika jana katika kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili hifadhi hizo.
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
UNESCO
kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya kale imeendesha warsha ya siku
moja kwa wakuu wa hifadhi na vivutio vya utalii hapa nchini huku wakuu
hao wakishirikishana mafanikio na changamoto zinazowakabili katika
hifadhi zao
Warsha
hiyo iliyohudhuriwa na Wakuu wa hifadhi mbalimbali hapa nchini iliweza
kuhusisha uwasilishaji wa mafanikio na changamoto wanazokutana nazo
wakuu wa hifadhi hizo katika hifadhi huku matatizo makubwa yakiwa ni
Ukosefu wa Pesa kwaajili ya Kujiendesha na Kwa baadhi ya hifadhi kukosa
nyumba za Wafanyakazi na upungufu wa wafanyakazi kwa baadhi ya hifadhi
hizo.
]Mbali
na Changamoto hizo pia wakuu wa hifadhi walielezea mafanikio yao katika
hifadhi hizo katika vipengele tofauti tofauti kama Vitendea kazi,
Ujumuikaji wa jamii katika hifadhi hizo, Utalii, Rasilimali watu,
Uhifadhi Utawala na mengineyo.
Moja
ya mafanikio katika nyanja tofauti Mkuu wa Hifadhi ya Usambara
Mashiriki (East Usambara Reserve Management) Bi Mwanaidi Kijazi alisema
kuwa hifadhi yake imetokea kuwa kituo cha Mafunzo kwa wengine na
kupelekea kuanzishwa kwa Amani Nature Reserve na hifadhi hiyo kufanikiwa
katika kutoa taarifa kwa wakati kwa njia ya Vipeperushi kuhusiana na
Mradi huo wa Amani Nature ambao upo kusini mwa Hifadhi hiyo ya Usambara
Mashariki.
Vilevile
alisema katika hifadhi yake kuna wafanyakazi ambao wanaweza kuhudhuria
shughuli za Hifadhi hiyo na kusema na hiyo ni moja ya Mafanikio katika
Hifadhi hiyo ya Usambara Mashariki.
Kwa
Upande wao UNESCO walisema wataendelea kushirikiana na idara ya Mambo
ya Kale katika kutoa ushirikiano na misaada ya kitaalam katika
kuhakikisha Hifadhi hizi zinaweza kujiendeleza na kujiboresha na kuvutia
watalii zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni