Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
akizungumza siku ya Alhamis Usiku, muda mfupi kabla ya kuonyeshwa kwa
filamu ya "the Boy from Geita" ambayo inaelezea uovu wanaotendewa watu
wenye ulemavu hususani watoto Nchi Tanzania. Katibu Mkuu Msaidizi wa
ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Bw. Ivan
Simonvic wapili kutoka kushoto alitambua mchango wa serikali katika
kuukabili uovu dhidi ya watu wenye ualibino na akahidi Taasisi hiyo
na nyingine za Umoja wa Mataifa ushurikiano na Serikali. wa Kwanza ni
Bw. Peter Ash mwanzilishi na Mkurugenzi wa Asasi ya Unter the Same
Sun na karibu na Balozi ni mwakilishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa
Canada katika Umoja wa Mataifa
Sehemu
wa wageni waalikwa waliofika kuangalia filamu ya "the Boy from Geita"
iliyonyeshwa Alhamisi usiku hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Mwandaaji
wa mwongozaji wa filamu ya "the Boy from Geita Bw Vic Sarin akizungumza
machache kuhusu kwanini aliamua kutengeneza filamu hiyo.
Sehemu nyingine ya waalikwa ambao pia walipata nafasi ya kuuliza maswali baada ya filamu hiyo.
Balozi akiteta jambo na Kijana huyu ( jina halikupatikana) raia wa Marekani mwenye ulemavu wa ngozi.
(ualibino)
Na Mwandishi Maalum, New York
SIKU
moja baada ya Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kuelezea kwa waandishi
wa habari juhudi zinazofanywa na serikali dhidi uovu
wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Kamisheni ya Haki
za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHR ) imesema itashirikiana
na Serikali ya Tanzania katika juhudi hizo za
kuukabili ouovu unaofanywa dhidi ya jamii hiyo ya watanzania.
Kauli
hiyo imetolewa Alhamisi usiku na Katibu Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya
Kamisheni ya Haki za Binadamu, Bw. Ivan Simonovic muda mfupi kabla
ya kuonyeshwa kwa filamu ya “ the Boy from Geita”.
Bw.
Ivan Simonovic amesema, ushirikiano huo ni katika kutambua juhudi
zinazofanywa na serikali katika siyo tu kwa kuhakikisha tatizo hilo
linatoweka lakini pia kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote
wanaohusika na ukatili huo.
“Tofauti
na nchi nyingine, Serikali ya Tanzania imeonyesha ujasiri na
uthubutu wa kukabiliana na uovu unaofanywa dhidi ya watu wenye
ualibino. Ni kwa kutambua juhudi hizo tutashirikiana na serikali
katika kukomesha uovu huu” akasema Bw. Simonovic.
Kauli
ya Bw. Ivan Simonovic ya kutambua juhudi hizo za serikali, kumetokana
na shuttle diplomacy iliyofanywa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania,
Balozi Tuvako Manongi ya kuonana na wakuu wa Idara ambazo
zimefadhili kuonyeshwa kwa filamu hiyo hapa Umoja wa Mataifa, pasipo
kuushirikisha wala kuujulisha Uwakilishi wa Tanzania.
Aidha maelezo
ya awali kuhusu filamu hiyo yanaupotoshaji wa baadhi ya mambo hali
iliyomfanya Mwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoj wa Mataifa
kuchukua fursa ya kuyatolea ufafanuzi.
“Usiku
huu ninapenda kutambua juhudi zinazofanywa na Moja ya nchi
Mwanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania, ambayo Mwakilishi
wake Wakudumu Balozi Tuvako Manongi yupo pamoja nasi. Siyo tu
kwamba Tanzania imeonyesha ujasiri na uthubutu wa kutambua ukubwa
wa tatizo linalowakumba watu wenye ualibino lakini pia imefanya
juhudi za kuwaelimisha wananchi wake huku ikuchukua hatua muhimu”
akasema Bw. Ivan Simonovic.
Akaeleza
zaidi kwamba kama watakavyoona kwenye filamu hiyo. Waziri Mkuu wa
Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amekuwa msemaji na mtetezi wa haki za
watu wenye ualibino kwa kufanya ziara za kutembelea maeneo mbalimbali
ya nchi kuhimiza na kuelimisha wananchi kuachana na ukatili huo.
“Kujituma
kwake na namna anavyolichukulia tatizo hili kwa uzito wa aina
yake, ni ushahidi wa namna gani Tanzania inavyokabiliana na
changatomo hii. juhudi hizi zimeleta matokeo chanya ambapo hakuta
taarifa za matukio ya kuvamiwa watu wenye ualibino katika miezi ya hivi
karibuni.
“
Ofisi ya Haki za Binadamu inakaribisha na kutambua juhudi hizo za
serikali ya Tanzania katika kukabiliana na Ubaguzi. Mfumo mzima wa Umoja
wa mataifa upo tayari kuwaunga mkono” akasema katibu Mkuu Msaidizi.
Alipopewa nafasi
ya kuzumgumza mbele ya hadhara hiyo. Balozi Tuvako
Manongi kwanza, alimshukuru Katibu Mkuu Msaidizi kwa kutambua
mchango wa serikali, na pia kumpatia fursa ya kuja kuzungumza na kutoa
fafanuzi kwa niaba ya serikali yake.
Balozi
Manongi, alirejea kauli aliyoitoa mbele ya waandishi siku ya
jumatano, kwamba, Tanzania haikatai na wala haipingi kwamba kuna tatizo
kwa watu wenye ualibino.
Akasema pamoja
na kukiri kuwapo kwa matukio ya uovu dhidi ya watanzania hao,
lakini angependa pia kuweka rekodi sawa na hasa kufuatia maelezo ya
upotoshaji ambayo yametolewa kwenye vipeperushi vinavyoitangaza filamu
hiyo.
Baadhi
ya mambo ambayo Balozi ameyatolea ufafanuzi ni lile linaloelezwa na
waandaji wa filamu hiyo kuwa eti ualibino ualianzia Tanzania miaka
2000 iliyopita jambo analosema halijathibitishwa kisayansi.
Akafafanua
pia kwamba, Watanzania ni waumini wa dini ya kiislamu au wakristo ,
kwa hiyo kusema kuwa sehemu kubwa ya watanzania wanaamini katika
uchawi halina mashiko.
Akasema
kwamba si sahihi pia kueleza kwamba wazazi ni washirika katika
kutenda maovu dhidi ya watoto wao wenye ualibino. Amefafanua pia kuwa
neno zeruzeru ni tafsri ya Kiswahili ya neno alibino na kwamba tafsri
inayotolewa na waandaji hao ni upotoshaji.
Balozi
Manongi pia amekanusha taarifa zilizoelezwa na waandaji hao kwamba
Asasi ya Under the Same Sun, ilipokuja Tanzania mwaka
2007 haikukuta chama chochote cha kuwasema watu wenye ualibino
si kweli. Kwani chama cha Tanzania Albinism Society ( TAS) kimekuwapo
tangu mwaka 1978 na kimekuwa kikiendesha shuguli zake kwa kushirikiana
na serikali.
“
Mashambulizi dhidi ya watu wenye ualibino nchini Tanzania, ni makosa
ya jinai, yanayofanywa na watu binafsi ambao wamejawa na mawazo uovu
ambayo yanaweza tu kuthibitishwa na vyombo yha sheria” akasisitiza
Balozi.
Na
kuongea kwamba Tanzania inaheshimu haki za binadamu na utawala wa
sheria na kwa kuheshimu huko haiwezi kutoa hukumu kiholela bila ya
kufuata mkondo wa sheria.
Akifafanua
Zaidi kwa takwimu Balozi Manongi amesema watu bilioni moja au Zaidi
wenye aina mbalimbali za ulemavu, asilimia 80 wanatoka nchi
zinazoendelea. Na kwamba kwa mujibu wa sensa ya watu
iliyofanyika nchini, watu 2.6 milioni sawa na asilimia 5.8 ya idadi
yote ya watu wana aina moja ama nyingine ya ulemavu. Kati yao 16,477 au
0.04 asilimia wana ualibino.
Wakati
wa kipindi cha majibu na maswali baadhi ya watizamaji walihoji sababu
ya waandaji wa filamu hiyo kuionyesha Marekani ili hali kwamba
katika Marekani yenyewe pia kuna vitendo vya ubaguzi wa hali ya
juu yakiwamo matukio ya watu kuuwa.
Wengine
walitaka kujua ni watu gani wanaonunua viungo vya watu wenye
ualibino swali lililojibiwa na waandaji wa filamu hiyo kuwa ni ni
matajiri wakiwamo wanasiasa kiuhalifu. Wakasema pia kwamba ni
watanzania wachache ambao bado wanaimani potofu dhidi ya watu wenye
ualibino, huku wakibainisha uhuru wa vyombo vya habari nchi Tanzania
imechangia kwa kiasi kikubwa kufahamika kwa madhila wanayofanyiwa watu
wenye ualubino.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni