BUKOBA VETERAN KUCHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI KESHO JUMAMOSI 17.10.2015 NA BUSWELU VETERAN

Bukoba Veteran kucheza mchezo wa Kirafiki kesho jumamosi 17.10.2015 kwenye Uwanja wa shule ya seminari ya Ntungamo Bukoba na Timu ya Buswelu Veteran kutoka Jijini Mwanza. Mtandao wa Bukobasports.com ukiongea na Nahodha wa Timu hiyo Kepteni Mwinyi Rajab umeelezwa kwamba mpambano huo wa kirafiki utapigwa kesho jioni na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Viwanja hivyo. Pia ameweza kuongeza kuwa kutapigwa mtanange mwingine wa kirafiki utaochezwa kesho yake jumapili 18.10.2015 kwenye Uwanja huo kuanzia 10:00 jioni. Bukoba Veteran Sports Club ni umoja wa wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara maskani yake yakiwa mjini Bukoba, Kagera.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Bukoba Veteran yenye maskani yake mjini Bukoba.
Maandalizi hayo ni pamoja na kujiandaa na Mtanange mkubwa wa Kirafiki kati ya Bukoba Veteran na Masaka Veteran utakaofanyika mwezi ujao tarehe 28.11.2015 huko Kampala Uganda.Wapenzi wa Soka Mjini Bukoba mnaombwa kujiokeza kwa wingi katika safari hiyo ya Masaka mwezi ujao na kwa kujua zaidi ya safari hiyo mnaombwa kuwasiliana na Uongozi wa Bukoba Veteran kupitia kwa Nahodha wa Timu hiyo au Viongozi wake.
Salum Bonge, Kepteni Mwinyi Rajab na Mohamed Kassimu(Moha")
Kepteni Mwinyi Rajab
Moha"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni