TECNO YAJA NA UBUNIFU ZAIDI


MAKAMPUNI yanayozalisha Simu nchini yameshauriwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu katika kusanifu na kuzalisha simu bora ili kwenda sambamba na soko na mahitaji ya wateja.

Wito huo umetolewa na Meneja mauzo wa simu za Tecno, Fred Kadilana wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu aina ya Phantom 5 uliofanyika Dar es Salaam juzi.

Kadilana alisema soko la bidhaa zao linakuwa kwa kasi hususan barani Afrika hivyo wanafanya jitihada kuhakikisha wanakwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia.

"Soko la simu za kisasa duniani linakuwa kwa kasi hivyo katika bidhaa zetu tunajitahidi kila kukicha kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya wananchi," alisema Kadilana.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Daniel Xu alisema falsafa ya kutengeneza simu bora ni kulenga mahitaji ya soko la dunia.

Alisema simu ya Phanthom 5 ni toleo linalowapa wateja usanifu wa kipekee wenye uwezo 32GB katika uhifadhi wa taarifa na pia 3 GB katika mfumo wa kusoma na kuperuzi katika simu kwa haraka zaidi.

"Simu hii ina uwezo wa 300m Ah katika betri lake hivyo kuondoa usumbufu wa kuchaji simu mara kwa mara," alisema Xu.


Xu alisema kutokana na changamoto zinazowakabili wateja wa simu za kisasa "Smartphone" kwa sasa, teleo hili linauwezo wa kumfanya mteja afurahie mawasiliano katika mazingira mbalimbali.

Aliongeza kuwa kwa kuzingatia ubora Tecno imeweza kushinda tuzo ya dunia kwa ubora na kwa sasa wanaongoza kwa mauzo kwa kipindi cha miaka mitano sasa barani Afrika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni