Dereva wa mbio za Langalanga Lewis
Hamilton amesherehekea ushindi wake wa Sochi Grand Prix kwa kumwagia
kidogo champagne rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa katika jukwaa la
washindi.
Baada ya kupatiwa taji la ushindi wa
mbio hizo zilizofanyika Urusi dereva Hamilton alianza kusherehekea
kama ilivyo utamaduni wake kwa kutikisa na kumwaga champagne
iliyokuwa kwenye chupa kubwa.
Rais Putin alimkabidhi Hamilton
kombe la ushindi baada ya kuimba wimbo wa taifa, na wakati akiondoka
Hamilton alianza kumwaga champagne kushangilia ushindi wake huo.
Lewis Hamilton akishangilia kwa kumwaga champagne iliyomwagikia rais Putin
Mamodo pia ilibidi waoge champagne kama inavyoonekana hapa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni