Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa chokozi katika uzinduzi wa mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini uliofanyika Hoteli ya New Africa Dar es Salaam leo asubuhi.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Makamba, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Msaidizi wa Balozi, Ubalozi wa UFINI ambao ni wafadhili wa mama misitu, Simo-Pekka Parviainen na Ofisa Mradi Ubalozi wa Finland, William Nambiza.
Mshauri wa Ufundi Weizara ya Maliasili na Utalii, Thomas Sellaine (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. |
Mkurugenzi Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Rahima Njaidi (kushoto), akielezea shughuli zinazofanywa na mtandao huo.
Mkuu wa Mradi ya Kilimo, Kipato na Ajira wa Shirika la Maendeleo la Uswisi, Ueli Mauderli (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
Mkutano wa uzinduzi huo ukiendelea.
Mwezeshaji, Faustine Ninga kutoka Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), akitoa maelekezo mbalimbali.
Meneja Kampeni Mama Misitu, Gwamaka Mwakyanjala (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
Balozi wa Mama Misitu, Asha Salimu (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
Wasanii walioigiza namna ya utunzaji wa miti. Kulia ni Philemon Robari na Mohammed Titima.
Maofisa mbalimbali waliopo kwenye mradi huo wa Mama Misitu wakiwa katika uzinduzi huo.
Na Mwandishi wetu.
MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.
MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.
Vipindi hivyo mfululizo vimetengenezwa katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Shirika la Kuendeleza Teknolojia za Asili (TATEDO) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuleta mabadiliko na kurasimisha sekta ya mkaa iweze kutoa ajira endelevu na kipato kwa jamii za vijijini na mijini.
Inakadiriwa kuwa mkaa na biashara za kuni huzalisha takriban (dola bilioni 1) za mapato kwa zaidi ya wazalishaji, wasafirishaji na wafanyabiashara laki tatu (300,000) katika mwaka 2012. Mahitaji ya mkaa nchini Tanzania yameongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa.
Mkaa endelevu ni mkaa unaozalishwa kwa njia endelevu kutoka katika Misitu ya Hifadhi ya Jamii bila kuchangia ukataji miti na uharibifu wa mazingira. Hata hivyo, uzalishaji wa aina hii ya mkaa bado haujajulikana. Kampeni hii mpya ina lengo la kuleta mabadiliko kupitia ubunifu wa vipindi mfululizo vya runinga ambavyo vinazinduliwa leo.
Nishati zitokanazo na tongamotaka (biomas) ni nishati muhimu sana nchini Tanzania itakayoendelea kutumika angalau zaidi ya miaka 20 ijayo. Kwa sasa, mkaa mwingi huzalishwa kinyume na utaratibu kutoka katika misitu ya hifadhi na misitu ya vijiji isiyo na mipango ya matumizi endelevu. Kutokana na usimamizi hafifu wa uzalishaji wa mkaa, imesababisha ukataji miti na uharibifu wa misitu kuongezeka nchini Tanzania.
Kampeni ya Mama Misitu na washirika wake (TFCG na MJUMITA) inalenga kuleta mabadiliko katika sekta ya mkaa kutoka tatizo kuwa fursa kubwa muhimu. Hivyo, vipindi vya runinga vya Mama Misitu pamoja na jumbe muhimu za mawasiliano zitasambazwa nchini Tanzania ili kuibua mjadala wa pamoja juu ya kuboresha utawala bora wa rasilimali misitu na kuleta faida kwa watanzania.
Mama Misitu ni kampeni ya mawasiliano yenye lengo la kuboresha utawala bora wa misitu ya Tanzania na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu ili watu wa Tanzania wanufaike zaidi na rasilimali misitu zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni