VYAMA VYA SIASA VYATAKIWA KUTUMIA LUGHA ZA KISTAARABU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Mkurugenzi wa Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Dr. Binadamu Hellen Bisimba   akizungumza na wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya Azaki Tanzania  katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyama  Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za binadamu na utawara bora,Bahame Nyanduga akizindua ilani ya uchaguzi ya Azaki Tanzania katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyama  Jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Hellen Bisimba na wakulia Mratibu wa Mtandao wa watetea wa haki za Binadamu Onesmo Ngurumwa.
 Wakionesha waandishi wa habari hawapo pichani  mara baada ya uzinduzi wa ilani ya uchauzi ya Azaki katika ukumbi  wa Milleniamu Towers Kijitonyam  Jijini Dar es Salaam.
 Bahame Nyanduga na Dr. Binadamu Hellen wakiteta jambo mara baada ya uzinduzi huo katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyama  Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi mbalimbali walio hudhulia uzinduzi huo katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyama  Jijini Dar es Salaam
 (Picha na Emmanuel Massaka)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 VYAMA vya Siasa vimeaswa kuachana na lugha ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani na badala yake vimetakiwa kunadi sera zao kwa wananchi waweze kupewa ridhaa inayotokana na kura.

Hayo ameyasema  Mwenyekiti wa Tume ya Haki ya binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga wakati wa uzinduzi wa ilani ya Asasi za Kiraia iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Nyanduga amesema wakati wa sasa ni kunadi sera kwa vyama vya siasa na sio kutumia lugha ambazo haziendani na Demokrasia wakati wa kuelekea uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  alitaja baadhi ya lugha zinazotumika ni pamoja na Tutashinda saa Nne Asubuhi, Goli la Mkono zote ni lugha ambazo hazitakiwi katika kuelekea katika uchaguzi mkuu.

Amesema kuwa vyombo vya dola ikiwemo jeshi la Polisi kuhakikisha linasimamia wananchi katika mchakato wa kuelekea katika uchaguzi pasipo kutumia nguvu ili wananchi waweze kusikiliza sera za vyama vyote kupitia wagombea wake.

Hata hivyo amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zilizosaini kuwepo kwa Mahakama ya ICC hivyo wale wote ambao watashiriki kuvunja amani wakati wa uchaguzi mkuu watahusika na mahakama hiyo kutokana na kufanya uchochezi na kuvuruga amani.

Aidha amesema kuwa wananchi nao wametakiwa kuvumiliana katika kipindi hiki pasipo kudharau chama cha mwenzake, uchanaji wa mabango  ya wagombea kwani hiyo sio demokrasia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni