WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AENDELEA KUPOKEA MISAADA YA VIFAA MBALIMBALI KUSAIDIA SHULE MPYA YA MSINGI KAKUNI MKOANI KATAVI

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda amepokea Msaada wa Vifaa vya Shule ikiwemo sare, Kompyuta pamoja na vifaa vya Michezo kutoka kampuni ya Huawei na Benki ya NMB.
 
Pinda amepokea misaada hiyo kutoka Kampuni hizo kwa lengo la kuzindua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Shule ya Msingi Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni Mkoani Katavi ni Shule aliyosoma Waziri Mkuu huyo Mhe,Mizengo Pinda.

Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukarabati madarasa ya Shule hiyo, barabara na Nyumba za Waalimu.

Meneja Uhusiano wa Huawei, Jin Liguo amesema msaada wa Kompyuta kutasaidia kuboresha Taaluma ya Wanafunzi hususani katika masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

Naye Afisa Mkuu wa fedha wa Benki amesema wametoa msaada huo kwa Shule alosoma Mhe,Mizengo Pinda ili kusaidia Watoto walio katika Shule hiyo katika Mavazi pamoja na vifaa vya Michezo ikiwemo Kompyuta. 
 
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu  Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa kompyuta mpakato zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni  iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi leo jijini Dar es salaam. Shule hiyo ya kisasa imeanzishwa kufuatia  wazo la Wazo la Waziri Mkuu, Mhe.Mizengo Pinda la kuwa na shule Bora na ya kisasa katika kijiji hicho na inajengwa kupitia michango na misaada ya wadau mbalimbali.
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu  Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa Tabuleti 100 zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni  iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.
 Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Bw. Waziri Barnabas akimkabidhi Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Tanzania sehemu ya msaada wa vifaa vya michezi vilivyotolewa na NMB kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.
 Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG) kilichopo mkoani Dodoma Bw. Salehe Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa Sare uliotolewa na kikundi hicho  kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni iliyopo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi .
  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na kampuni hiyo kusaidia elimu katika shule mpya ya msingi Kakuni mkoani Katavi, ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 30 vilivyotolewa na Benki hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni