RAFIKI WA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS ASEMA MWANARIADHA HUYO AMEDHOOFIKA

Rafiki wa mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amebainisha kuwa mwanariadha huyo amedhoofika, amekonda na kuvunjika moyo wakati huu akitumikia kifungo cha miaka 5 jela.

Kauli ya rafiki huyo imekuja wakati Pistorius anayetumikia adhabu hiyo kwa kumuua bila ya kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013, akiwa anangojea uamuzi wa kusamehewa ili akamalizie hukumu yake nyumbani.
                          Marehemu Reeva akiwa na Pistorius wakati wa uhai wake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni