Hii taarifa imegusa Vichwa vya Habari vya Vyombo vingi vya habari Duniani, inahusu ajali ambayo imetokea wakati watu wakiwa ndani ya Msikiti Mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia ambako waumini wengi wa Dini ya Kiislamu huwa wanakwenda kwa ajili ya Hijjah.
Ajali hiyo inahusisha winch kubwa ambalo lilikuwa likitumiwa kwenye ujenzi eneo la jirani na Msikiti huo kuangukia Msikiti huo, ambapo kwa wakati huo kulikuwa na watu zaidi ya 800 wakiendelea na sala ndani ya Msikiti.
Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa watu wanaoenda kwenye Msikiti huo kutokana na maeneo yanayozunguka Msikiti kuna majengo mengi yanayoendelea kujengwa na kukarabatiwa pamoja na Msikiti wenyewe kufanyiwa ukarabati wa upanuzi ili kuweza kungiza watu wengi zaidi.
Mpaka sasahivi Ripoti zinaonesha zaidi ya watu 100 wamefariki, wengine zaidi ya 200 wamepata majeraha na Mamlaka za Mji huo wanasema sababu hasa za winch hilo kuanguka inatokana na upepo mkali pamoja na mvua kubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni