Mwenyekiti
 wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza 
kushoto) akiwa kwenye hali ya furaha mara baada ya kuzindua msimu wa 
saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 
mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja 
na Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio
 warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (mwenye shati jeupe), Afisa 
Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. 
Salim Kimaro (wa pili kulia) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano 
NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
 Meneja
 Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) warataibu wa mbio 
hizo Bw Erasto Kilawe (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa 
habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio
 za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu 
katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  Wengine ni pamoja na 
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa pili
 kushoto), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya 
Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa tatu kushoto).
 Afisa
 Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. 
Salim Kimaro (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo 
kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City 
Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa 
CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la 
Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) na Bi Ummy 
Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa
 mbio hizo.
Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti
 wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua msimu wa
 saba wa mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika Novemba 15 mwaka huu
 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mbio 
za Rock City Marathon, zinazoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus 
International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT), 
pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) zinalenga kutambua na 
kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani 
kupitia sekta ya michezo.
Akizungumza
 katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Bw. 
Malinzi alisema baraza linafuraha kuona makampuni binafsi yakijiingiza 
katika kuinua mchezo wa riadha nchini.
“Mchezo
 wa riadha una changamoto kubwa na tunatambua jitihada zinazoendelea 
kufanywa na kampuni ya Capital Plus katika kurudisha hadhi ya mchezo 
 huu nchini kama ilivyokuwa miaka ya sabini na themanini,” alisema.
 Alisema
 kuwa Tanzania itarudi kileleni katika medani za michezo duniani kama 
wachezaji wataandaliwa katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
“Inashangaza
 kuona taifa la watu milioni 45 linawakilishwa na wanariadha wachache 
sana, tena katika mbio ndefu huku tukikosa wanariadha wanaoliwakilisha 
vyema taifa katika mbio fupi,” alisema.
Akizungumza
 katika hafla hiyo, Meneja Mkuu kutoka kampuni ya Capital Plus 
International, Bw. Erasto Kilawe alisema kuwa mbio hizo zimekuwa 
zikionyesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.
 “Jiji
 la Mwanza limebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii. Jambo 
hili limetusukuma kuendelea kumulika vivutio vya kipekee vinavyopatikana
 katika ukanda wa ziwa Victoria kupitia mbio hizi,” alisema Bw. Kilawe 
huku akiongeza kuwa mikakati kabambe imewekwa ili kuhakikisha mbio za 
mwaka huu zinakuwa za mafanikio makubwa kuliko misimu iliyopita.
Alisema
 baadhi ya makampuni yameanza kujitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni 
pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Precision Air, 
New Africa Hotel na Bank M huku makampuni zaidi yakionyesha nia ya 
kudhamini mbio hizo.
“Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.
Uzinduzi
 huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na 
wanariadha, viongozi wa vyama vya riadha, viongozi wa Baraza la Michezo 
la Taifa (BMT) na wadau mbali mbali wa riadha nchini.
Kwa 
upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF , Salim Kimaro alisema 
kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kudhamini mbio hizo kutokana 
ari yao katika kukuza hali ya michezo hapa nchini.
“Kwetu
 suala la michezo ni moja ya vipaumbele vyetu kutokana na ukweli kuwa 
michezo ni afya na pia ni sehemu ya ajira kwa vijana kwa sasa…tunaahidi 
kuwa mstari wa mbele katika kufaanikisha mbio hizi,’’ alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni