
Baadhi
 ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven 
a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi 
sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu 
kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika 
mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao 
tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale 
wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.PICHA ZOTE NA MICHUZI 
JR-IRINGA

 Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha 
Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa 
Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni 
uliofanyika.
 Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha 
Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa 
Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni 
uliofanyika  ndani ya uwanja wa Samora mkoani 
Iringa.
  Katibu
 wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu 
zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa
 kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya 
rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda  nafasi ya Urais.
 
 Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli
 alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka 
huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka 
mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
 Dkt
 Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la 
Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni 
uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.
 Baadhi
 ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye 
mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli, kwenye uwanja 
wa Samora mkoani Iringa.
 Magufulika
 staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa 
nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa 
wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi 
hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga 
push up kama ionekanavyo pichani.
 Mgombea
 Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo 
Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani
 Iringa.
  Dk
 Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu 
Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
 Vimbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda
wazee
 wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt 
Magufuli uliofanyika  katika Mji wa Ilula Jimbo la 
Kilolo mkoani Iringa.
  Mjumbe
 wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa 
mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa 
kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
 Wananchi
 wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za 
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia .
 Wananchi
 wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt
 Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 
25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze 
kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano













Hakuna maoni:
Chapisha Maoni