Waziri
mkuu wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiwa anakata
utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua magari ya kubeba wagonjwa ambayo
ameyakabidhi leo mkoani Arusha kwa ajili ya kupelekwa wilayani
Ngorongoro kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya kubeba wagonjwa Picha na manyaraleo blog
waziri pinda akiwasili katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha
Waziri mkuu akielekea kukabidhi rasmi magari mawili ya kubebea wagonjwa
mkuu
wa mkoa wa Arusha akiongeozana na waziri mkuu kwa ajili ya makabidhiano
ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoletwa na waziri
habari picha na Mahmoud Ahmad,Arusha
Waziri mkuu
wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda leo amekabithi
magari mawili ya kubebea wagonjwa yenye dhamani ya shilingi milioni
150.
Magari
hayo ambayo yamekabidhiwa, yametokana na ahadi ambayo waziri huyo alitoa
Kwa Wananchi wa wilaya ya ngorongoro wakati Alipofanya ziara wilaya ni
humo september 2013.
Akizungumza
wakati akikabidhi magari hayo waziri mkuu Mizengo Pinda alisema wakati
alipokuwa kwenye ziara wilaya ni humo, alipokea malalamiko ya
kutakuwepo na magari ya kubebea wagonjwa hali ambayo ili mfanya atoe
ahadi nasasa ameamua kuitekeleza.
"nilipata
malalamiko nikapeleka wizara ya afya, wakapokea na kaniambia watafanyia
kazi sasa Kila nikiwauliza Wakaniambia bado sasa nikabahatika kupata
safari ya Kwenda japani nilipoenda Nitakuja na na Wananchi wa Tanzania
wa naishi uko nikawaomba wa nisaidie japo gari moja ya kubebea wagonjwa
sasa wao ndio wakaja wakanipa magari haya mawili "alisema pinda
Alisema
Kuwa mara baada ya kupokea magari hayo aliyafanyia ukarabati mdogo na
sasa ameamua kuyaleta Mkoani ili yapelekwe katika wilaya husika ambapo
alisema Kuwa mara baada ya kufikishwa wilaya ni ngorongoro gari moja
litatumika katika hospitali ya waso huku ingene ikitumika hospitali ya
Enduleni.
Aidha aliwataka viongozi wa wilaya ya ngorongoro kutumia vyema magari hayo haswa katika shughuli
iliolegwa, Pamoja na kuyatunza ili ya weze kutumika na kubeba wagonjwa
wakati Mgonjwa anapotokea au tatizo la gafula linapotokea.
Aidha
alibainisha Kuwa magari haya ameyatoa yeye mwenyewe kutoka Kwa wa
fadhili na sio magari ya wizara hivyo wakapokee haya wakijua ni ahadi ya
waziri mkuu, na sio ya wizara hivyo wapokee haya wakati wakiwa Wana
ngoja magari ya kubebea wagonjwa kutoka wizarani
Alipokea
msaada huo mkuu wa wilaya ya ngorongoro Ashimu Mgandila alisema Kuwa wa
nashukuru sana Kwa msaada hii kwani Wananchi haswa wakina mama waja wa
zito wali Kuwa wanateseka sana wakati walipo Kuwa wa naumwa.
Alisema Kuwa wali Kuwa na gari ya kubebea wagonjwa lakini imearibika Kwa kipindi karefu ila hii itakuwa ni suluisho Kwa Wananchi wa wilaya hiyo.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngorongoro John
kulwa alisema Kuwa magari haya ni ukumbozi hasa Kwa upande wa wamama
Pamoja na wagonjwa mahututi kutaka katika Kila kata na Kila kaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni