MAJAMBAZI WANNE WAULIWA JANA USIKU JIJINI ARUSHA

Image result for kamanda sabas

 
Mahmoud Ahmad wa manyaraleo blog
WATU watatu wanaosadikiwa ni majambazi ambao ni  raia wa Kenya  pamoja
na Mtanzania mmoja wameuwa katika majibizano na polisi eneo la
Chekereni mpakani mwa wilaya ya Arumeru na Jiji la Arusha.

Aidha majambazi hayo yamekufa kwasababu ya ushirikiano kati ya jambazi
mmoja aitwaye Sixtus Ngowi (51) ambaye alikamatwa awali na kutoa
ushirikiano kwa polisi kuwa anashirikiana na wenzake hao watatu raia
wa Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini hapa, Kamanda wa Polisi
Mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema polsi walipokea taarifa za
kiintelijensia Agosti 19 /2015 juu ya kuwepo kwa kundi la majambazi
wanaotoka nchini Kenya na kuja Mkoani Arusha kwa lengo la kufanya
uporaji kwakushirikiana na majambazi wenzao hapa nchini.

Alisema kutokana na taarifa hizo polsi walizifuatilia na kufanikiwa
kumkamata Ngowi mkazi wa Ngulelo Jijini Arusha na baada ya mahojiano
kwa kina ,Ngowi alikiri kuwa yeye ni miongoni mwa majambazi ambaye
anashirikiana na majambazi hao kutoka nchini Kenya na kufanya matukio
mbalimbali nchini Tanzania.

Marehemu Ngowi alikiri kuhusika na tukio la uporaji kwenye kampuni ya
Security Group 4 akiwa na wenzake na kuiba dola za Kimarekani
2,000,000 Jijini Dar es Salaama mwaka 2005  na baadaye kufikishwa
mahakamani.

Lakini pia mwaka 2002 Ngowi pamoja na wenzake  alihusika katika tukio
la uvamizi kwenye benki ya NBC Tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro mbali
na matukio hayo mwaka 2014  Machi aliwahi kushtakiwa Nchini Kenya
katika mahakama ya Kilimani Law Court Jijini Nairobi lakini baadaye
aliachiwa huru.

Ngowi kabla ya kwenda na polisi kufanikisha mtego wa majambazi wenzake
wa Kenya aliwataja kwa jina moja moja baadhi ya majambazi aliokuwa
akishirikiana nao kuwa ni Kamau, Bon, Mike, Kim, Katiwa na wengine
ambao alisema hawajui kwa majina lakini wanatokea nchini Kenya huku
hapa nchini alimtaja mshirika wake aitwaye Richard mkazi wa Dar e s
Salaam.

Pia Ngowi aliendelea kukiri kushirikiana na wenzake kuhusika kwenye
matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika Jiji la Arusha
yaliyotokea juni 23/2015 na Agosti 17/2015 ambapo walengwa walikuwa ni
wafanyabiashara wakubwa wanaojihusiha na biashara ya madini ya
Tanzanite na Hoteli za Kitalii.

Miongoni mwa wafanyabiashara hao ni pamoja na Mathias Manga ambaye ni
Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC)  ambaye
alijeruhiwa kwenye ubavu wa kulia kwa risasi katika jaribio la kupora
fedha na madini na alipokuwa kwenye muendelezo wa mahojiano jambazi
huyo aliahidi kushirikiana na polisi kupatikana kwa wenzake.

Na siku ya juzi Septemba 17/2015 wakiwa kwenye mpango wa kuvamia
mojawapo ya duka ya kubadilisha fedha liitwalo sanya la Jijini hapa
,Ngowi alikubali kuongozana na askari kwaajili ya kufanikisha
kupatikana kwa wenzake lakini kabla ya kuwakamata walipofika eneo la
Chekereni majambazi hao raia wa Kenya  walishtuka kuwa  walioongozana
na mwenzao ni askari polsi na wao kuanxa kupiga risasi na kufanikiwa
kumjeruhi Ngowi aliyekuwa katika gari nyingine iliyokuwa na polisi hao
na alikufa akipelekwa hospitalini.

Baada ya tukio hilo polisi waliamua kujibu mapigo na kufanikiwa
kuwauwa watu watatu ambao ni Simon Kariuki, Bonifas Mbulu na Thadeo
Njuguna  huku wengine wakitoroka ambao walikuw akatika gari namba
T981AVK aina ya Noah.

Katika eneo la tukio ilibainika kuwa majambazi hao watatu kila mmoja
alikutwa na bastola pamoja na risasi , magegi matatu meusi ambapo
baada ya kuyafungua walikuta bunduki aina ya AK 47 mbili zenye namba
83LG 3953 56-1 na nyingine yenye maandishi ya kirusi na SMG namba 56-1
28038394 ,bastola tatu zenye namba CZ 75 Compact Luger- 9mm  namba
a.269206, CZ 85 B LUGER 9mm namba 051967 na Chines Pistol namba
967741, magazine nne za ziada tupu za smg, risasi 85 za SMG /Ak 47 na
risasi 28 za bastola.

Vitu vingine walivyokutwa navyo ni Radio Call mbili aina ya Kenwod na
Charger moja zilizokuwa hewani na mawimbi ya polisi Arusha, Bullet
Proof moja, vifaa vya kusafisha Bunduki (Gunslick), tochi kubwa tatu,
mbili kati a hizo ni aina ya DP na moja ni Panasonic, mashuka ya
kimasai matatu ,mifuko mitau ya kubebea fedha ,gloves za vitambaa
,kofia mbili aina ya boshori ambazo katika tukio la kumvamia
mfanyabiashara aitwaye Manga zilitambulia pia kulikutwa na koti moja
lenye muenekano wa sare za kijeshi.

Pia marehemu hao watatu raia wa Kenya walikutwa na vitambulisho vitatu
vya nchini Kenya veyen majina ya Simon Kariuki, Bonifas Bulu na Thadeo
Njuguna na kitambulisho kimoja cha UN-ICTR  chenye jina la Chacha
marwa , leseni ya udereva iliyotolewa Kenya yenye jina la Thadeo
Njuguna, Kadi ya Benki ya Equity, Master Card yenye jina la Somon
Githinji pamoja na kadi ya benki ya Cooperative baki yenye jina la
Thadeo Njuguna simu tano aina ya Nokia , Tecno na Samsung.

Polisi wanaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo pamoja na kuwatafuta
watuhumiwa wengine ambao walitoroka katika tukio na kubaini mtandao wa
majambazi hao kwani kwa mujibu wa polisi kuwa  kwataarifa alizozitoa
Ngowi kabla ya kufa zinadai kuwa majambazi hao wa Kenya walitumwa na
wenzao ambao wanatumikia vifungo kutokana na wizi wa beni za NBC na
NMB Moshi Mkoani Kilimanjaro na kuhukumiwa vifungo waliwatuma kutafuta
fedha ili familia zao ziweze kuendelea kuishi wakiwa wanaendelea
kutumikia vifungo .

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Mery
kwaajili ya utambuzi kutoka kwa ndugu na jamaa zao wa karibu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni