Jaji mmoja nchini
Marekani amemuagiza afisa wa Kentucky kufungwa jela kwa kukaidi amri
ya mahakama baada ya kugoma mara mbili kutoa hati ya ndoa kwa
wanandoa mashoga.
Afisa huyo Bi. Kim
Davis amesema kuwa kwa imani yake ya Kikristo atakuwa amefanya kosa
lisilo na msamaha kwa kukubali kutia saini katika hati ya ndoa ili
kuridhia ndoa hiyo ya wanandoa mashoga.
Hata baada ya Jaji
kusema kuwa atamuachia huru Bi. Davis ambaye ni karani mkuu iwapo
atatoa ruhusa kwa makaimu wake kusaini hati ya ndoa hiyo ya mashoga,
bado alikataa kutoa ruhusa hiyo.
Mahakama Kuu ya
Marekani iliridhia ndoa za mashoga kukubalika kisheria nchini
Marekani tangu mwezi Juni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni